
Tuma picha au yaliyomo mengine kwenye kifaa kingine kwa kutumia Bluetooth
Tumia Bluetooth ili kutuma picha, video, kadi za biashara, na maudhui mengine
yaliyoundwa na wewe kwenye kompyuta yako au simu au kifaa kinachotangama cha
rafiki.
1 Chagua kipengee cha kutuma.
2 Chagua
Chaguzi
>
Tuma
>
Kupitia Bluetooth
.
3 Chagua kifaa ili kuunganisha. Ikiwa kifaa kinachohitajika hakijaonyeshwa, ili
kukitafuta, chagua
Utafutaji upya
. Vifaa vya Bluetooth vilivyo karibu huonyeshwa.
4 Kama kifaa kile kingine kinahitaji msimbo wa kibali, ingiza msimbo wa kibali.
Msimbo wa kibali, ambao unaweza kufasili mwenyewe, lazima uingizwe katika
vifaa vyote. Msimbo wa kibali katika vifaa vingine huwa vimewekwa. Kwa maelezo
zaidi, angalia mwongozo wa mtumiaji wa kifaa.
Msimbo wa kibali ni halali tu kwa muunganisho wa sasa.
Chaguo zinazopatikana zinaweza kutofautiana.
20
Uunganikaji