Kuhusu muunganisho wa Bluetooth
Chagua
Menyu
>
Mipangilio
>
Uunganikaji
>
Bluetooth
.
Tumia Bluetooth ili kuuunganisha bila waya kwa vifaa vinavyotangamana, kama vile
vifaa vingine vya rununu, kompyuta, vifaa vya kichwa, na vifaa vya gari.
Unaweza pia kutuma vipengee kutoka kwa kifaa chako, kunakili mafaili kutoka PC yako
inayotangamana, na kuchapisha kwa kutumia printa inayotangamana.
Bluetooth hutumia mawimbi ya redio ili kuunganisha, na vifaa lazima viwe kati ya mita
10 (futi 33) ya ile nyingine. Vizuizi, kama vile kuta au vifaa vingine vya elektroniki,
vinaweza kusababisha muingiliano.