Misimbo ya ufikivu
Msimbo wa PIN au
PIN2
(dijiti 4-8)
Hizi hulinda SIM yako dhidi ya matumizi yasiyodhinishwa au
yanayohitajika ili kufikia vipengee vingine.
Unaweza kuweka simu yako kukuuliza msimbo wa PIN wakati
unapokiwasha.
10
Utumizi wa kawaida
Kama haijapeanwa pamoja na SIM yako au ulisahau misimbo,
wasiliana na mtoa huduma wako.
Ukicharaza msimbo usio sahihi mara tatu mfululizo, unahitaji
kufungua msimbo na msimbo wa PUK au PUK2.
Msimbo wa PUK au
PUK2
(dijiti 8)
Hizi zinahitajika ili kufungua msimbo wa PIN au PIN2.
Kama haijapeanwa pamoja na SIM yako, wasiliana na mtoa
huduma wako.
Nambari ya IMEI
(dijiti 15)
Hii hutumiwa ili kutambua simu halali katika mtandao. Nambari
inaweza pia kutumiwa ili kufunga, kwa mfano, simu zilizoibiwa.
Huenda pia ukahitaji kupeana namba ya huduma za Nokia Care.
Ili kuona nambari yako ya IMEI, piga *#06#.
Msimbo wa kufunga
(msimbo wa
usalama)
(isiyozidi dijiti 5)
Hii hukusaidia kulinda simu yako dhidi ya matumizi
yasiyoruhusiwa.
Unaweza kuseti simu yako kukuuliza msimbo wa kufunga
ambao unafasili. Msimbo mbadala wa kufunga ni 12345.
Tunza msimbo kwa siri na katika mahali salama, kando na simu
yako.
Ukisahau msimbo na simu yako kifungwe, simu yako itahitaji
huduma. Gharama za ziada huenda zikatumika, na data zote
za kibinafsi katika simu yako huenda zikafutika.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Nokia Care au muuzaji wa simu
yako.