Nokia C2 05 - Ingiza SIM kadi na betri

background image

Ingiza SIM kadi na betri

Zingatia: Zima kifaa na usiiunganishe na chaja au kifaa kingine chochote kabla ya

kubandua vifuniko vyovyote. Epuka kugusa visehemu vya elektroniki wakati wa

kubadilisha vifuniko vyovyote. Daima hifadhi na kutumia kifaa kikiwa na vifuniko vyake

vimewekwa.

Muhimu: Kifaa hiki kimeundwa ili kutumiwa na SIM kadi wastani tu (angalia mfano).

Utumizi wa SIM kadi zisizotangamana huenda kukaharibu kadi au kifaa, na huenda

kukaharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi. Tafadhali shaurinan na opereta wa

rununu yako kwa utumizi wa SIM kadi ambayo ina mkato wa mini-UICC.

Muhimu: Kuzuia SIM kadi kuharibika, daima ondoa betri kabla ya kuingiza au

kuondoa kadi.

Simu hii inakusudiwa kutumiwa na betri ya BL-4C. Daima tumia betri halisi za Nokia.

SIM kadi na sehemu zake za kuunganishia zinaweza kuharibika kwa urahisi kwa

mikwaruzo au kukunjwa, kwa hiyo kuwa muangalifu wakati wa kuishika, kuingiza au

kuondoa kadi.

1 Weka kidole chako katika kona iliyo juu ya simu, na kwa makini inua na uondoe

kifuniko cha nyuma (1).

2 Kama betri imeingizwa, indoa betri (2).

3 Ingiza au ondoa SIM kadi (3 au 4). Hakikisha eneo la mguso la kadi linaangalia chini.

6

Namna ya kuanza

background image

4 Lainisha maeneo ya kugusa ya betri na chumba cha betri, na uingize betri (5).

Kubadilisha kifuniko cha nyuma, elekeza vishiko vya kufunga vya chini kuwadia

sehemu zao (6), na ubonyeze chini hadi kifuniko kiingine mahali pake (7).