
Ingiza kadi ya kumbukumbu
Tumia tu kadi za kumbukumbu zinazoendana zilizoidhinishwa na Nokia kwa ajili ya
kutumiwa na kifaa hiki. Kadi zisizoendana zinaweza kuharibu kadi na kifaa na kuharibu
data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Simu yako inakubali kadi za kumbukumbu zenye uwezo wa hadi 32 GB.
Namna ya kuanza
7

1 Ondoa kifuniko cha nyuma.
2 Hakikisha eneo la mguso la kadi ya kumbukumbu linaangalia chini, na uingize SIM
kadi. Sukuma kadi ndani, hadi ijifunge.
3 Badilia kifuniko cha nyuma.
Ondoa kadi ya kumbukumbu
Muhimu: Usiondoe kadi ya kumbukumbu wakati programu tumizi inaitumia.
Kufanya hivyo kunaweza kuharibu kadi ya kumbukumbu na kifaa na kuharibu data
iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Unaweza kuondoa na kubadilisha kadi ya kumbukumbu bila kuzima simu.
1 Ondoa kifuniko cha nyuma.
2 Sukuma kadi ndani, hadi ijiachilie, na vuta kadi nje.
3 Badilia kifuniko cha nyuma.