Nokia C2 05 - Vifaa vya matibabu

background image

Vifaa vya matibabu
Utumiaji wa kifaa kinachotoa mawimbi ya redio, ikiwa ni pamoja na simu zisizotumia waya, kunaweza kuingiliana na utendakazi

wa vifaa vya kitabibu ambavyo havijalindwa kikamilifu. Mwone daktari au mtengenezaji wa kifaa hicho cha kitabibu kujua

kama vimelindwa kikamilifu dhidi ya nishati ya mawimbi ya redio ya nje.

Vifaa vya matibabu
Watengenezaji wa vifaa vya matibabu hupendekeza utenganisho wa angalau sentimeta 15.3 (inchi 6) kati ya kifaa

kisichotumia waya na kifaa cha matibabu mwilini, kama vile kirekebisha mapigo ya moyo na vifaa vingine vinavyohusiana na

moyo ili kuepuka uwezekano wa mwingiliano na kifaa hicho cha kimatibabu. Watu ambao wana vifaa kama hivyo wanapaswa:

Daima weka kifaa kisichotumia waya kwa umbali wa sentimeta 15.3 (inchi 6) kutoka kwa kifaa cha matibabu.

Usibebe kifaa kisichotumia waya katika mfuko wa shati.

Shikilia kifaa kisichotumia waya kwenye sikio kando na kifaa cha matibabu.

Zima kifaaa kisichotumia waya ikiwa kuna sababu yoyote ya kushuku kwamba mwingiliano unafanyika.

Fuata maagizo ya mtengenezaji kwa kifaa cha matibabu mwilini.

Ikiwa una maswali yoyote kuhusu kutumia kifaa chako kisichotumia waya na kifaa cha matibabu mwilini, wasiliana na mtoa

huduma wako wa afya.