Mazingira yenye uwezekano wa milipuko
Zima kifaa chako katika eneo lenye mazingira yenye uwezekano wa milipuko, kwa mfano karibu na pampu za gesi kwenye
vituo vya mafuta. Cheche katika maeneo kama hayo zinaweza kusababisha mlipuko au moto unaoweza kuleta majeraha ya
mwili au kifo. Fuata masharti kwenye vituo vya mafuta, maeneo ya kuhifadhi na kugawia mafuta, viwanda vya kemikali au
mahali ambapo shughuli za ulipuaji zinaendelea kufanyika. Maeneo yenye mazingira yenye uwezekano wa milipuko mara
nyingi lakini si mara zote yanakuwa na alama zilizo wazi. Inajumuisha chini ya sitaha ya boti, maeneo ya usafirishaji au ya
kuhifadhi kemikali na maeneo ambayo hewa ina kemikali au chembechembe kama vile nafaka, vumbi au poda ya chuma.
Unapaswa kuwasiliana na watengenezaji wa magari yanayotumia mafuta aina ya gesi oevu ya petroli iliyoyeyushwa (kama
vile propeni au buteni); ili kuamua ikiwa kifaa hiki kinaweza kutumiwa vizuri katika maeneo yao.