Mazingira ya kutumia
Kifaa hiki kinaafikia maongozi ya ujiwekaji wazi wa masafa ya redio katika mkao wa utumizi wa kawaida kwenye sikio au
angalau sentimeta 1.5 (inchi 5/8) mbali na mwili. Kikasha chochote cha kubebea, kishikiza kwenye mkanda, au kishikizi cha
matumizi ya kuvaliwa mwilini, kinatakiwa kisiwe na chuma na kinatakiwa kuweka bidhaa hii angalau umbali uliotajwa hapo juu
kutoka kwenye mwili wako.
Kutuma faili za data au ujumbe uhitaji unganiko na mtandao wenye ubora wa hali ya juu. Faili za data au ujumbe zinaweza
kucheleweshwa hadi unganisho huo upatikane. Fuata maagizo ya umbali wa kutenganisha hadi upitisho ukamilike.