Nokia C2 05 - Magari

background image

Magari
Mawimbi ya redio (RF) yanaweza kuathiri mifumo ya eletroni iliyo ndani ya gari ambayo imewekwa vibaya au haijalindwa

kikamilifu, kwa mfano utemaji wa mafuta kieletroniki; kufunga breki kieletroniki, kidhibiti mwendo kieletroniki, na mifuko ya

hewa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mtengenezaji wa gari lako au vifaa vyake.

Watu wenye ujuzi na sifa zinazotakiwa tu ndio wanaweza kukarabati au kuweka kifaa ndani ya gari. Usakinishaji au huduma

mbaya inawezakuwa hatari na inaweza kubatilisha waranti yako. Hakikisha mara kwa mara kwamba vifaa vyote visivyotumia

waya ndani ya gari vimefungwa vizuri na vinafanya kazi sawasawa. Usihifadhi au kubeba vimiminika vinavyoweza kuwaka,

gesi au vitu vyenye kulipuka kwenye kichumba kimoja na kifaa hiki, sehemu zake au vifaa vyake vya ziada. Kumbuka kwamba

mifuko ya hewa hujaa hewa kwa nguvu kubwa. Usiweke kifaa chako au viboreshaji kwenye eneo ambalo mfuko wa hewa

hutumika.