Nokia C2 05 - Habari ya utoaji cheti (SAR)

background image

Habari ya utoaji cheti (SAR)
Kifaa hiki cha mkononi kinatimiza maelekezo yanayohusu ujiwekaji wazi kwa mawimbi ya redio.

Kifaa chako cha mkononi ni transmita na kipokezi cha redio. Imesanifiwa isizidi viwango vya juu vya ujiwekaji wazi kwa nishati

ya frikwensi za redio vilivyopendekezwa na maelekezo ya kimataifa. Maelekezo haya yalitayarishwa na shirika huru la

kisayansi ICNIRP na yanajumuisha viwango vya tahadhari ya ziada iliyowekwa kuhakikisha usalama wa watu wote, bila kujali

umri wala afya.

Maelekezo ya ujiwekaji wazi kwa ajili ya vifaa vya mkononi hutumia kizio cha kipimo kijulikanacho kama Kiwango Maalum cha

Ufyonzaji ( ‘Specific Absorption Rate, au SAR’ ). Kiwango cha juu cha ‘SAR’ kilichoelezwa kwenye maelekezo hayo ya ICNIRP

ni 2.0 wati/kilogramu (W/kg) kilichotokana na wastani wa gramu 10 za tishu. Vipimo kwa ajili ya ‘SAR’ hufanyika kwa kutumia

mikao ya matumizi ya kawaida na kifaa kikiwa kinatumika kwa kiwango chake cha juu cha nguvu kilichosajiliwa kwenye

frikwensi za bendi zote zilizojaribiwa. Kiwango halisi cha ‘SAR’ cha kifaa wakati kinatumika kinaweza kuwa chini ya kiwango

cha juu kabisa kwa sababu kifaa kimesanifiwa kutumia kiasi kile cha nguvu inayohitajika tu kufika kwenye mtandao. Kiasi

hicho hubadilika kutegemea sababu kadhaa kama vile ukaribu wa kituo cha mtandao.

Kiwango cha juu cha SAR kwenye maelekezo ya ICNIRP wakati wa kutumia kifaa karibu na sikio ni W/kg 0.60.

Matumizi ya vifaa vya ziada yanaweza kusababisha viwango tofauti vya SAR. Viwango vya ‘SAR’ vinaweza kutofautiana

kutegemea matakwa ya nchi kuhusu utoaji taarifa na upimaji na bendi ya mtandao. Taarifa zaidi kuhusu SAR inaweza

kupatikana chini ya taarifa ya bidhaa kwenye www.nokia.com.

38

Maelezo ya bidhaa na usalama