Nokia C2 05 - Kuhusu Usimamiaji haki za Dijito (‘Digital Rights Management’)

background image

Kuhusu Usimamiaji haki za Dijito (‘Digital Rights Management’)
Unapokuwa ukitumia kifaa hiki, tii sheria zote na heshimu utamaduni wa wenyeji, uhuru binafsi wa mtu na haki halali za

wengine, ikiwemo hakimiliki. Kinga za hakimiliki zinaweza kukuzuia dhidi ya kunakili, kurekebisha au kuhamisha picha, muziki

na vitu vingine.

Wamiliki wa vilivyomo wanaweza kutumia aina tofauti za teknolojia za usimamiaji haki za kidijito (‘digital rights management’

- DRM) kulinda haki zao za ubunifu, zikiwemo hakimiliki. Kifaa hiki kinatumia aina anuai za maunzi laini ya DRM ili kuingia

kwenye vitu vinavyolindwa na DRM. Kwa kutumia kifaa hiki unaweza kufikia vilivyomo vilivyolindwa na WM DRM 10 na OMA

DRM 1.0. Ikiwa baadhi ya maunzi laini ya DRM yameshindwa kulinda vilivyomo, wamiliki wa vilivyomo wanaweza kuomba

kwamba uwezo wa maunzi laini hayo ya DRM ya kuingia kwenye vitu vipya vinavyolindwa na DRM ubatilishwe. Ubatilishwaji

huo unaweza pia kuzuia uwekwaji upya wa vitu vinavyolindwa na DRM ambavyo tayari viko kwenye kifaa chako. Ubatilishwaji

wa maunzi laini hayo ya DRM hauathiri matumizi ya vitu vinavyolindwa na aina nyingine za DRM au matumizi ya vitu

visivyolindwa na DRM.

Vitu vinavyolindwa na usimamiaji haki za kidijito (DRM) huja na leseni ambayo huainisha haki zako za kutumia vilivyomo.

Kama kifaa chako kina vitu vinavyolindwa na WMDRM, leseni na vilivyomo vikipotea kama kumbukumbu ya kifaa ikifomatiwa.

Unaweza pia kupoteza leseni na vilivyomo ikiwa mafaili kwenye kifaa chako kikiharibika. Kupoteza leseni au vilivyomo

kunaweza kupunguza uwezo wako wa kutumia vilivyomo vilevile kwenye kifaa chako tena. Kwa taarifa zaidi, wasiliana na

mtoa huduma wako.

Maelezo ya bidhaa na usalama

35