
Kuhudumia kifaa chako
Shughulikia kifaa chako, betri, chaja na vifaa vya ziada kwa uangalifu. Mapendekezo yafuatayo yatakusaidia kulinda matakwa
ya dhamana yako.
•
Weka kifaa kikiwa kikavu. Taka za mtuamo, unyevu wa hewa na aina zote za vimiminiko au unyevu zinaweza kuwa na
madini yanayoweza kutia kutu saketi za elektroniki. Kifaa chako kikilowana, ondoa betri na kiruhusu kifaa kikauke
kabisa kabla ya kurudisha betri tena.
•
Usitumie au kuhifadhi kifaa chako kwenye maeneo yenye vumbi au uchafu. Sehemu zake zinazosogea na vijenzi vya
elektroniki vinaweza kuharibika.
•
Usihifadhi kifaa kwenye hajijoto ya juu au ya chini. Joto la juu linaweza kufupisha maisha ya vifaa vya elektroniki,
kuharibu betri, na kukunja au kuyeyusha aina fulani za plastiki.
•
Usihifadhi kifaa kwenye halijoto baridi. Wakati kimerudi kwenye joto lake la kawaida, unyevunyevu unaweza
kutengenezeka ndani ya kifaa, ambao unaweza kuharibu bodi za saketi za eletroni.
•
Usijaribu kufungua kifaa zaidi ya jinsi ilivyoelekezwa kwenye mwongozo huu.
•
Antena, kufanya mabadiliko au kuweka viambatisho visivyoidhinishwa kunaweza kuharibu kifaa hiki na kunaweza
kukiuka sheria zinazoendana na vifaa vya redio.
•
Usiangushe, kugonga au kutikisa kifaa hiki. Kushika vibaya kunaweza kuvunja bodi za umeme na ufundi wa ndani.
•
Tumia kitambaa laini, kisafi na kikavu kusafisha uso wa kifaa hiki.
•
Usipake rangi kifaa. Rangi inaweza kuziba sehemu zake zinazosogea na kuzuia utendaji kazi mzuri.
•
Zima kifaa na uondoe betri mara kwa mara kwa utendakazi bora.
•
Weka kifaa chako mbali na sumaku au maeneo ya sumaku.
•
Kuweka data zako muhimu zikiwa salama, zihifadhi angalau sehemu mbili tofauti, kama vile kwenye kifaa chako, kadi
ya kumbukumbu, au kompyuta, au andika chini maelezo muhimu.