Nokia C2 05 - Usalama wa betri

background image

Usalama wa betri
Daima zima kifaa na ondoa unganiko kwenye chaja kabla ya kuondoa betri. Unapochopoa chaja au kifaa chochote cha ziada,

kamata na uvute plagi na siyo waya.

Wakati chaja yako haitumiki, ichomoe kwenye plagi ya umeme na kwenye kifaa. Usiache betri iliyochajiwa kabisa ikiwa

imeunganishwa kwenye chaja, kwa sababu uwekaji wa chaji ya ziada kunaweza kufupisha maisha ya betri. Ikiachwa bila

kutumika, betri iliyokuwa imejaa chaji itapoteza chaji yake kadri muda unavyopita.

Daima jaribu kuweka betri kwenye halijoto kati ya 15°C na 25°C (59°F na 77°F). Halijoto ya juu sana hupunguza uwezo na

uhai wa betri. Kifaa chenye betri moto au baridi kinaweza kisifanye kazi kwa muda.

Mkato wa umeme unaweza kutokea kwa bahati mbaya kama kitu cha chuma kweneye betri, kwa mfano, ukibeba betri ya

ziada mfukoni. Mkato wa umeme kwenye temino huweza kuharibu betri au hicho kinachounganisha.

Usitupe betri zilizokwishatumika kwenye moto kwa sababu zinaweza kulipuka. Tupa betri kwa kufuata sheria za mahali ulipo.

Rejeleza betri pale inapowezekana. Usitupe kama takataka za kawaida za nyumbani.

Usichanechane, kukata, kufungua, kugongesha, kukunja, kuharibu, au kupasua seli au betri. Katika tukio la betri kuvuja,

usiruhusu umaji wa betri kugusana na ngozi au macho. Hii ikifanyika, osha maeneo yaliyoathirika mara moja na maji, au tafuta

msaada wa kitabibu.

Usirekebishe, kutengeneza tena, kujaribu kuingiza vitu geni kwenye betri, au kuingiza au kuweka wazi kwa maji au umiminiko

mwingine. Betri zinaweza kulipuka kama zimeharibika.

Tumia betri na chaja kwa matumizi yaliyokusudiwa tu. Utumiaji mbaya, au utumiaji wa betri au chaja isiyotangamana inaweza

kuleta hatari ya moto, mlipuko, uvujaji, au hatari zingine, na huenda ukabatilisha kibali chochote au waranti. Kama unaamini

betri au chaja imeharibika, ipeleke kwa kituo cha huduma ifanyiwe uchunguzi kabla ya kuendelea kuitumia. Kamwe usitumie

betri au chaja yoyote iliyoharibika. Tumia chaja ndani ya nyumba tu.