Nokia C2 05 - Taarifa ya betri na chaja

background image

Taarifa ya betri na chaja
Kifaa chako kimekusudiwa kutumiwa na betri inayoweza kuchajiwa upya ya BL-4C . Nokia inaweza kutengeneza modeli za

ziada za betri zipatikane kwa kifaa hiki. Daima tumia betri halisi za Nokia.

Kifaa hiki kimekusudiwa kutumika kinapopokea umeme kutoka kwa chaja zifuatazo: AC-3 . Namba asili ya modeli ya chaja

ya Nokia huenda ikatofautiana kulingana na aina ya chomeka, inayotambuliwa na E, X, AR, U, A, C, K, B, au N.

Betri inaweza kuchajiwa na kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye itachoka. Wakati muda wa kuongea na muda wa

kusubiri unaonekana wazi kuwa mfupi kuliko kawaida, badilisha betri.