Nokia C2 05 - Uchakataji

background image

Uchakataji

Wakati simu hii imefika mwisho wa maisha yake, nyenzo zake zote zinaweza kufufuliwa

kama nyenzo na nishati. Ili kuhakikisha utupaji sahihi na utumizi mwingine, Nokia

hushirikana na wenzi wake kupitia mpango unaoitwa Sisi:tunachakata upya. Kwa

maelezo juu ya kuchakata upya bidhaa zako za zamani za Nokia na wapi unaweza

kupata maeneo ya mkusanyiko, nenda kwa www.nokia.com/werecycle, au piga simu

kwa Kituo cha Mawasiliano cha Nokia.

Chakata upya kifurushi na miongozo ya mtumiaji kwa mpango wa uchakati upya wa

eneo lako.

Alama ya pipa iliyo na mkato kwenye bidhaa, maandishi, au kifurushi chako

hukukumbusha kwamba bidhaa zote za elektroniki, betri, na vilikimbizi umeme lazima

zipelekwe kwenye mkusanyiko tofauti wakati bidhaa inapokwisha. Hitaji hili linatumika

katika Jumuiya ya Ulaya. Usitupe bidhaa hizi kama takataka zisizochambuliwa za

manispaa. Kwa maelezo zaidi juu ya sifa za simu yako kwa mazingira, nenda kwa

www.nokia.com/ecoprofile.